Mama Pendo alifungua gunia la kwanza la tangawizi na hakuhitaji mizani kujua kuna tatizo.
Aliingiza mkono ndani, akachukua vipande viwili, akavinusa halafu akamwangalia Nasma.
“Hii imepata unyevu.”
Nasma akachukua kipande kimoja.
Harufu haikuwa mbaya sana, lakini ilikuwa nzito kuliko kawaida. Hakukuwa na ukavu mkali waliotarajia kabla ya kusaga.
“Sehemu gani ya stock?”
“Rack ya nyuma.”
“Batch card?”
Mama Pendo akamuita worker mmoja.
“Hamisi, leta cards zote za tangawizi.”
Ghala la KVK lilikuwa limejaa vitu ambavyo kwenye karatasi vinaweza kuonekana kama mali: magunia ya pilipili, tangawizi, mdalasini, turmeric, cartons tupu, rolls za labels, packaging bags na sealed products zilizokuwa zinasubiri dispatch.
Lakini siku hiyo Nasma hakuona mali.
Aliona maswali.
Gunia linaweza kuuzwa?
Packaging hii inafaa product gani?
Batch hii ina customer?
Stock hii inaweza kuwa cash ndani ya siku ngapi?
Yusuf aliingia akiwa na clipboard.
“Tumefunga count ya pilipili?”
“Nusu.”
“Na tangawizi?”
“Simama hapo.”
Nasma akamwonyesha sample yenye unyevu.
Yusuf akakunja uso.
“Ni magunia mangapi?”
“Bado hatujui.”
“Kwa vitabu?”
“Vitabu vinaonyesha stock. Havionyeshi smell.”
Mama Pendo akasema, “Ndiyo maana leo hamtakaa ofisini.”
Walifungua magunia moja baada ya jingine.
Magunia mawili yalikuwa salama.
La tatu lilikuwa na unyevu chini.
La nne lilikuwa bora lakini limeanza kubadilika rangi.
Nasma akaweka alama pembeni.
“Separate. Hakuna kinachoingia grinder mpaka quality check.”
Yusuf akauliza, “Hii ni loss yote?”
“Tusikimbie. Tunajua damaged quantity kwanza.”
Waliweka mizani katikati ya ghala.
Worker akasoma kilograms. Mama Pendo akaandika. Nasma akalinganisha na batch card. Yusuf akatoka rack moja kwenda nyingine.
Baada ya saa moja, tofauti ya inventory ikaanza kuonekana.
Si theft.
Si gunia lililopotea kwa siri.
Mchanganyiko wa waste ambayo haikuandikwa kwa usahihi, moisture loss, packaging rejects na stock ambayo karatasi bado ilikuwa inaonyesha kama usable.
Yusuf akasema, “Hii ndiyo Khalfan alikuwa anasema haifanani?”
“Partly.”
Mama Pendo akamwangalia. “Na kuna packaging ya family pack pale nyuma. Nyingi sana.”
Walitembea mpaka rack ya mwisho.
Kuna bundles nyingi za bags kubwa zilizo-printiwa miezi iliyopita. Product hiyo ilikuwa imepangwa kwa customer ambaye sasa alikuwa amepunguza orders.
Yusuf akashika bundle moja.
“Hizi nazo ni asset.”
“Ndio,” Nasma alisema.
“Na zinalipiwa.”
“Ndio.”
“Basi why hazitusaidii?”
“Kwa sababu customer wa size hii ameshuka.”
Yusuf akaangalia bundles hizo tena.
“Packaging hii inaweza kutumika kwa product nyingine?”
“Brand line na weight imeprintiwa.”
“Kwa hiyo tuna mali ambayo haiwezi kugeuka cash bila customer huyo.”
Mama Pendo akasema, “Au bila kuuza kwa loss kwa mtu wa repackage.”
Nasma akaandika kwenye loss/slow-moving sheet.
Yusuf hakusema kitu kwa muda.
Waliendelea kuhesabu.
Cartons za small packs zilikuwa chache.
Sealing film ya packs ndogo ilikuwa karibu kuisha.
Pilipili raw stock ilikuwa ya kutosha kwa batch mbili kubwa au batches nyingi ndogo.
Nasma akaenda kwenye whiteboard ya production.
“Tunabadilisha mix.”
Mama Pendo akauliza, “Kwa nini?”
“Small packs zina-turn faster sokoni. Tunaweza kuuza kwa shops ndogo na cash cycle ni fupi.”
Yusuf akasema, “Margin?”
“Per kilo inaweza kuwa higher, lakini labor na packaging cost inaongezeka.”
Mama Pendo akatikisa kichwa. “Na packing line itabanwa. Small packs ni kazi nyingi kuliko cartons za restaurant.”
“Tunafanya batches chache. High-turnover products only.”
“Na old restaurant order?”
“Tutatengeneza corrective sample na quantity ndogo tuliyo-confirm. Hatutajaza stock ya product ambayo demand yake imeanguka.”
Yusuf akasogea karibu na board.
“Hii inamaanisha slow customer atachelewa.”
“Ndio.”
“Utaambia?”
“Nitaambia kabla hajauliza.”
Mama Pendo akacheka. “Hapo umeanza kuwa mama yako kidogo.”
Nasma akageuka.
Mama Pendo akainua mkono. “Sijasema uwe yeye. Nimesema hiyo ilikuwa habit yake nzuri.”
Nasma akatabasamu kidogo.
Walifungua batch cards za miezi mitatu.
Saada alipougua, production planning ilikuwa imeanza kuwa reactive. Orders zikichelewa, Nasma alisogeza batches. Packaging ili-orderwa kulingana na customer promises ambazo baadaye zilipungua. Waste records hazikuingia siku hiyo hiyo.
Yusuf akasema, “Nilikuwa naona ghala limejaa na nafikiria kampuni ina pesa.”
Nasma akamwangalia.
“Na sasa?”
Yusuf akachukua gunia moja lililowekwa upande wa damaged stock.
“Nilikuwa nahesabu magunia. Sikuwa nahesabu kama yanaweza kuuzwa.”
Nasma hakutumia sentensi hiyo kama ushindi.
Aliandika tu kwenye sheet:
**Physical stock ≠ saleable stock.**
Yusuf akaona.
“English?”
“Kwa sababu Khalfan anapenda labels zake.”
“Usimlaumu.”
Mchana, Nasma alipiga simu kwa customer aliyekuwa anasubiri product ya old mix.
“Tutachelewa siku mbili,” alisema.
“Kwa nini?”
“Tumefanya stock review. Raw material ya batch yako ipo, lakini tuna prioritize order yenye confirmed dispatch na tunafanya quality correction.”
“Saada aliahidi Ijumaa.”
“Ninajua.”
“Basi mama yako alipanga tofauti.”
Nasma alifumba macho kwa sekunde.
“Na hali ya stock ya leo ndiyo ninayoweza kukupa. Naweza kukupa half batch Ijumaa, balance Jumatatu.”
Mteja hakufurahia.
Lakini alikubali half batch.
Nasma akaandika commitment kwenye board.
Kila uamuzi ulikuwa na gharama.
Ukihifadhi stock kwa customer anayelipa haraka, unamchelewesha mwingine.
Ukitoa raw material kwa batch ya margin ndogo, unakosa high-turnover packs.
Ukiweka workers wengi kwenye packing, payroll pressure inaongezeka.
Hakuna option iliyokuwa safi.
Jioni, Khalfan aliingia na laptop yake.
Aliangalia loss sheet, physical counts na old inventory summary.
“Hii ndiyo mismatch,” alisema. “Books zilikua na stock value juu kuliko usable stock.”
Yusuf akauliza, “Kwa kiasi gani?”
Khalfan akasema, “Sijafunga reconciliation. Lakini enough kwamba tusitumie inventory value kama argument ya kusema company ni rich.”
Nasma akasema, “Na supplier shipment?”
Khalfan akasogeza screen.
“High-turnover mix unayotaka inahitaji zaidi ya stock ya Sudi. Especially tangawizi salama.”
Yusuf akasema, “Na invoice yake ndiyo tunajaribu kuchelewesha.”
“Exactly.”
Mama Pendo akavua gloves.
“Kwa hiyo tumegundua stock yetu si nyingi kama tulivyodhani, na ili tuuze faster tunahitaji stock mpya ambayo hatujalipia.”
Khalfan akasema, “Hiyo ndiyo business sentence ya leo.”
Yusuf akakaa kwenye sack moja.
“Mjomba akiiona hii atasema tuuze machine.”
Nasma akajibu, “Na ndiyo maana kesho tunahitaji cash-flow map, si argument.”
Alifunga loss register mpya.
Kwenye cover akaandika:
**DAMAGED / SLOW-MOVING / UNUSABLE — PHYSICAL CHECK REQUIRED.**
Mama Pendo akasema, “Hii register itabaki?”
“Ndiyo.”
“Si kwa sababu ya family dispute tu?”
“Hapana. Kila month.”
Mama Pendo akatikisa kichwa.
“Good. Mama yako alikuwa anaamini sana kichwa chake.”
Nasma akatabasamu kwa huzuni.
“Na mimi pia.”
“Basi wote mmejifunza.”
Walipokuwa wanafunga ghala, simu ya Nasma ikaita.
Sudi.
Aliangalia clock.
Deadline yao ya saa sabini na mbili ilikuwa karibu.
Akapokea.
“Nasma.”
“Ndio.”
“Niliona partial payment imeingia kidogo.”
“Kesho tuna cash map na Khalfan. Nataka kukupa proposal kamili.”
Sudi akasema, “Kesho jioni.”
“Nimekuelewa.”
“Nasma, naomba usiniletee story ya mali, stock, customers, na mama yako. Mimi nina wakulima waliotoa bidhaa.”
“Sitaleta story. Nitaleta mpango.”
Sudi akakaa kimya kwa sekunde.
Kisha akasema, “Kesho jioni nataka mpango wa malipo, si maelezo.”
---